Psalms 28

Kuomba Msaada

(Zaburi Ya Daudi)


1 aNinakuita wewe, Ee Bwana, Mwamba wangu;
usiwe kwangu kama kiziwi.
Kwa sababu ukinyamaza
nitafanana na walioshuka shimoni.

2 bSikia kilio changu unihurumie
ninapokuita kwa ajili ya msaada,
niinuapo mikono yangu kuelekea
Patakatifu pa Patakatifu pako.


3 cUsiniburute pamoja na waovu,
pamoja na hao watendao mabaya,
ambao huzungumza na jirani zao maneno mazuri,
lakini mioyoni mwao wameficha chuki.

4 dWalipe sawasawa na matendo yao,
sawasawa na matendo yao maovu;
walipe sawasawa na kazi za mikono yao,
uwalipe wanavyostahili.

5 eKwa kuwa hawaheshimu kazi za Bwana,
na yale ambayo mikono yake imetenda,
atawabomoa na kamwe
hatawajenga tena.


6 f Bwana asifiwe,
kwa maana amesikia kilio changu
nikimwomba anihurumie.

7 g Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu,
moyo wangu umemtumaini yeye,
nami nimesaidiwa.
Moyo wangu unarukaruka kwa furaha
nami nitamshukuru kwa wimbo.


8 h Bwana ni nguvu ya watu wake,
ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake.

9 iWaokoe watu wako na uubariki urithi wako;
uwe mchungaji wao na uwabebe milele.
Copyright information for SwhKC